Katibu mkuu wa muungano wa utamaduni Malindi, MADCA Joseph Karisa Mwarandu amewasuta vikali baadhi ya viongozi wa kaunti ya Kilifi kwa kususia sherehe za kumuenzi shujaa Mekatilili wa Menza.
Akizungumza wakati wa maadhimisho ya kila mwaka huko Shakahola eneo bunge la Magarini kaunti ya Kilifi, Mwarandu amesema kitendo hicho kinadhihirisha kuwa viongozi hao wameuacha utamaduni na kuashiria kupungua kwa uzalendo ndani yao.
Kwa upande wake Katibu mkuu wa chama cha Mau Mau humu nchini Gitu Wa Kahengeri amewatolea mwito viongozi nchini kukumbatia na kuuenzi utamaduni ili kuzidi kuendelea uzalendo.
Kwenye maadhimisho hayo, Kahengeri aliweka jiwe la msingi kwa ujenzi wa makavazi ya shujaa mekatilili wa Menza yatakayotumika kumkumbuka shujaa huyo na kuvutia watalii wa kitaifa na kimataifa.
Taarifa na Charo Banda.