Viongozi wa kisiasa katika eneo la Ganze wametakiwa kushirikiana katika kutatua masaibu ya ardhi.
Kiongozi wa maswala ya kimaendeleo katika jamii Daniel Mangi amesema kuwa wanasiasa waliwaahidi wananchi kuwa watatatua masaibu ya ardhi ambayo yameshuhudiwa kwa miaka mingi.
Mangi ameutaja mzozo wa ardhi ya Giriama Ranch kama mzozo unaohitaji kuingiliwa kati kwa haraka na viongozi.
Mangi amesema kuwa wananchi wamekuwa wakifurushwa kutoka kwa mashamba yao ambayo mabwenyenye wamedai kuyamiliki bila viongozi wao kutilia maanani masaibu yao.
Taarifa na Marietta Anzazi.