Story by Our Correspondents –
Viongozi wa Muungano wa OKA wamefanya kikao cha faraga kutathmini ripoti ya kamati inayosimamia mipango ya ndani ya Muungano huo, kuhusu ni nani kati ya viongozi hao anafaa kupewa bendera ya Muungano huo kuwania kiti cha urais.
Viongozi hao akiwemo Kinara wa Chama cha WIPER Kalonzo Musyoka, Moses Wetangula wa Ford-Kenya na Gideon Moi wa KANU amekutana katika hoteli moja mjini Naivasha kuitathmini kwa kina ripoti hiyo.
Kinara wa Chama cha ANC Musalia Mudavadi amekosa kuhudhuria mkutano huo huku wadadisi wa maswala ya kisiasa wakisema hatua hiyo ya Mudavadi huenda ikachangia Muungano huo kusambaratika.
Mkutano huo uliohudhuriwa na aliyekuwa Gavana wa Kiambu William Kabogo na Kinara wa Chama cha Narc-Kenya Martha Karua aliyetuma mwakilishi wake kuichambua ripoti hiyo ambayo inadaiwa kuegemea upande wa Kalonzo Musyoka kupeperusha bendera ya Muungano huo kuwania urais.