Story by Bakari Ali –
Baadhi ya Viongozi wa chama cha ODM katika kaunti ya Mombasa waanza maandalizi ya mkutano wa Muungano wa Azimio la Umoja utakaofanyika katika uwanja wa Tononoka siku ya Jumapili.
Mwenyekiti wa chama hicho kaunti ya Mombasa Mohammed Hamid Khamis amewataka viongozi wa kisiasa watakayohudhuria mkutano huo kuweka kando tofauti zao za kisiasa na kuunga mkono sera za Kinara wao Raila Odinga za kuingia Ikulu.
Akiunga mkono kauli hiyo, Mgombea wa kiti cha eneo bunge la Nyali Said Abdallah amewahimiza wanasiasa wenza kudumisha utulivu wakati wa mkutano huo.
Kwa upande wake, Mbunge wa Jomvu Badi Twalib amewataka wakaazi wa kaunti ya Mombasa kujitokeza kwa wingi katika mkutano huo ili kufanikisha malengo ya Odinga kuingia Ikulu.