Story by: Salim Mwakazi.
Viongozi wa muungano wa One Kenya Alliance OKA wakiongozwa na kinara wa chama cha WIPER Kalonzo Musyoka wameendeleza msururu wa mikutano ya kisiasa hii leo kilele cha mikutano hio ikifanyika eneo la Lunga lunga kaunti ya Kwale.
Akizungumza wakati wa mikutano hio Kalonzo amekanusha madai yanayoenezwa kwamba alifanya mazungumzo ya faragha na kinara wa mungano wa azimio la Umoja Raila Odinga katika kaunti ya Mombasa.
Kalonzo aliyekua ameandamana na viongozi wenza wa muungano huo akiwemo kinara wa KANU Gideon Moi, mwenyekiti wa WIPER balozi Chirau Ali Mwakwere na viongozi wengine amesema watatoa muelekeo wa kisiasa hivi karibuni.