Baadhi ya viongozi katika kaunti ya Lamu wanailamu serikali kuu kwa kile wanachodai kama kushindwa kudhibiti visa vya dhulma dhidi ya wanawake nchini.
Wakiongozwa na mjumbe maalum katika bunge la kaunti ya lamu Bi. Amina Kale, viongozi hao wamedai kwa sasa visa vya unyanyasaji miongoni mwa wanawake vimeongeza huku idara husika za kiserikali zikiwa zimelifumbia macho tatizo hili.
Kwa upande wake mwakilishi mwengine maalum katika bunge la kaunti ya Lamu Bi. Jane Ndungu ameitaka serikali kuu kupitia idara za usalama kuwachukulia hatua wote wanaojihusisha na visa hivi.
Taarifa na Hussein Mdune