Story by Mwanaamina Fakii –
Baadhi ya viongozi wa kaunti ya Kwale wamemkosoa aliyekuwa Mwenyekiti wa tume ya kitaifa ya ardhi Dkt Mohamed Swazuri kwa madai kwamba alishindwa kumaliza utata wa ardhi katika ukanda wa pwani licha ya kupewa jukumu hilo.
Wakiongozwa na Mwakilishi wadi ya Mwavumbo kaunti ya Kwale Joseph Ndeme, viongozi hao wamesema Dkt Swazuri alishindwa kuibuka na suluhu la kudumu kwa mizozo ya ardhi Pwani wakati alipoongoza tume hiyo ya kitaifa ya ardhi.
Ndeme ameilaumu serikali ya kitaifa kwa kushindwa kuwasaidia wananchi kupata hati miliki za ardhi zao na kumaliza migogoro ya ardhi huku akipendekeza kubuniwa kwa sheria muafaka zitakazomaliza mizozo ya ardhi katika ukanda wa Pwani.
Wakati uo huo ameitaka idara ya Mahakama nchini kutobukali kutumiwa visivyo na baadhi ya mabwenyenye walio na malengo potovu ya kuwanyanyasa wananchi ardhi zao.