Story by Our Correspondents-
Vyama vya kisiasa vya Jubilee, ODM, KANU, Wiper vimeungana na kubuni Muungano wa kisiasa unaofahamika kama Azimio One Kenya Coalition.
Katika kikao cha pamoja cha makatibu mkuu wa vyama hivyo kilichoandaliwa jijini Nairobi wakiongozwa na Msemaji wa Raila Odinga Prof Makau Mutua, viongozi hao wamesema wamekubaliana kwa kauli moja kubuni Muungano huo.
Akizungumza na Wanahabari katika kikao hicho, Katibu mkuu wa chama cha ODM Edwin Sifuna amewakosoa wale wanaofurahia kuharamishwa kwa BBI, akisema bado kuna maswala tata ambayo hayajatatuliwa huku akidokeza kwamba Muungano huo ndio utakaoshinikiza mabadiliko.
Naye Katibu mkuu wa chama cha Wiper Shakila Abdallah amesema wametia saini mkataba maelewano ambao utachangia wakenya wote kunufaika na ambao utachangia amani na utangamano katika kampeni za uchaguzi mkuu.
Kwa upande wake Katibu mkuu wa chama cha Jubilee Jeremiah Kioni amesema mkataba huo waliotiwa saini unalenga kuwasaidia wakenya na kutimiza ndoto za viongozi waliotangulia pamoja na malengo ya Rais Uhuru Kenyatta kwa wakenya.