Viongozi wa Kike humu nchini, wameapa kutoshiriki kwenye mageuzi ya Katiba wakihofia kuwa huenda mabadiliko hayo yakahujumu nafasi zao kama viongozi.
Wakiongozwa na Mwakilishi wa Kike kaunti ya Kilifi Getrude Mbeyu, viongozi hao wamesema hawapo tayari kushiriki kwenye mazungumzo ya mageuzi ya Katiba, wakidai kuwa kubadilishwa kwa katiba kutaathiri pakubwa nafasi ya Wanawake katika uongozi.
Akizungumza mjini Mombasa, Getrude amesema mageuzi ya katiba yanayopigiwa debe humu nchini huenda yakahujumu utendekazi wa wanawake mashinani.
Kauli yake imeungwa mkono na Mwakilishi Maalum wa bunge la kaunti ya Kilifi Elizabeth Mbuche aliyesema kama viongozi wanawake hawaungi mkono hatua ya kuondoa nyadhfa za Uwakilishi wa wanawake nchini.
Taarifa na Charo Banda.