Viongozi wa kiislamu katika eneo la ukunda kaunti ya Kwale wamepokea mafunzo kuhusu jinsi ya kujikinga na maambukizi ya viruis vya Corona kabla ya nyumba za ibada kufunguliwa.
Akizungumza na Wanahabari baada ya mafunzo hayo yalioandaliwa katika shule ya msingi ya Mwakigwena, Mwenyekiti wa Baraza kuu la mashauri ya Kiislamu KEMNAC Sheikh Juma Ngao amesema mafunzo hayo yasaidia kudhibiti maambukizi.
Sheikh Ngao amesema tayari mikakati ya kufanikisha ibada kwa kuzingatia masharti ya kiafya, ikiwemo watu kuvaa barakao, kukaa umbali wa mita moja kutoka kwa wengine ni kati ya mikakati ambayo imepewa kipao mbele.
Wakati uo huo ameitaka serikali kufungua shule ya mafunzo ya utalii ya Ronald Ngala katika eneo la Vipingo kule kaunti ya Kilifi ili kuwawezesha wanafunzi kupata mafunzo hayo na kuiboresha sekta ya utalii.