Viongozi wa dini ya Kislamu kule mjini Mombasa wamehimizwa kuungana pamoja ili kuhakikisha wanawahamasisha vijana kuhusu maadili na mafunzo ya dini.
Sheikh wa Msikiti wa Dar-Ulum katika eneo la Likoni Juma Bega, amesema vijana wengi hawana elimu ya kutosha kuhusu mafunzo ya dini ndiposa wanajikuta wakifanya mambo maovu.
Akizungumza na Wanahabari, Bega ameitaka serikali ya kaunti ya Mombasa kuwasaidia viongozi wa dini hiyo kuunda vikao vya mafunzo ya dini hususan kukafini maiti ili kuhakikisha yanaleta muongozo bora katika jamii.
Kauli yake imeungwa mkono na Sheikh Swaleh Ibrahim ambaye amesema idadi ni ndogo mno ya wazee wanaohusika na taratibu hizo katika eneo la Likoni na Mombasa huku akisema nia aibu mno kwa vijana wenye umri mdogo.
Taarifa na Hussein Mdune.