Story by Hussein Mdune-
Baadhi ya viongozi wa kidini kaunti ya Mombasa wamewataka viongozi wa kisiasa kukoma kuingiza siasa katika swala la mpango wa serikali wa kuagiza Mahindi ya GMO wakidai kwamba swala hilo linafaa kujadiliwa kwa njia mwafaka.
Viongozi hao wakiongozwa na Askofu wa Kanisa la Ushindi Baptism eneo la Likoni Joseph Maisha wamesema wakati huu Kenya inapitia hali ngumu ya uchumi na kuna haja ya kuunga mkono wazo hilo.
Amesema uagizaji wa vyakula vya GMO unatekelezwa vizuri katika taifa la Afrika Kusini hivyo basi kama vyakula hivyo vitaletwa humu nchini vitakabiliana na uhaba wa chakula.
Kauli yake inajiri siku chache tu baada ya Kiongozi wa upinzani nchini Raila Odinga kudai kwamba vyakula vya GMO sio vizuri kwa afya ya wakenya.