Story by Hussein Mdune-
Huku joto la kisiasa likionekana kushamiri humu nchini baadhi ya viongozi wa kidini wamejitokeza na kuwataka wanasiasa kukoma kueneza siasa za chuki na ukabila.
Viongozi hao wa kidini wakiongozwa na Askofu wa Kanisa la ushindi Baptist Joseph Maisha wamesema siasa za chuki na ukabila huenda zikachangia taifa hili kushuhudia migawanyiko ya kijamii.
Askofu Maisha amehoji kwamba kuna haja ya viongozi kueneza ujumbe wa amani wakati huu ambapo taifa linaelekea katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2022 ili kuepukana na vuruga.
Wakati uo huo amewataka wanasiasa kutowashurutisha wananchi kuwachagua kwa maslahi yao binafsi na badala yake kuwapa nafasi kufanya maamuzi ya busara.