Picha kwa hisani –
Padre wa Kanisa Katoliki la St Michael katika Parokia ya Kiganjo eneo la Chaka kule kaunti ya Nyeri Samuel Njigua amewahimiza Viongozi wa kisiasa nchini kutekeleza majukumu waliopewa ya uongozi ili kufanikisha miradi ya maendeleo.
Akizungumza wakati wa ibada ya Misa ya Jumapili katika Kanisa Katoliki la St Michael eneo la Chuka kule kaunti ya Nyeri, Padre Njigua amesema hatua hiyo itasaidia pakubwa kuzitatua changamoto mbalimbali nchini.
Padre Njigua amewaomba pia waumini wa dini ya kikristo kuendelea kuliombea taifa hili ili kuepuka changamoto mbalimbali ikwemo uogonjwa hatari ya virusi vya Corona.
Akihutubia waumini wa Kanisa hilo baada ya kuhudhuria ibada Misa ya Jumapili, Rais Uhuru Kenyatta ameahidi kuboresha sekta ya biashara katika eneo la Chaka, kuboresha muundo msingi sawia na kuboresha maenndeleo.
Kiongozi wa taifa amewahimiza wakenya kuendelea kuliombea taifa hili kuwa taifa la amani na umoja huku akiwahimiza wakenya kushikamana kama jamii moja kwa kuzingatia demokrasia na Katiba ya nchi.