Story by Salim Mwakazi–
Baadhi ya viongozi wa kidini nchini wamejitokeza na kumtetea Rais Uhuru Kenyatta na Raila Odinga kwa kuungana pamoja ili kuhakikisha taifa hili linashuhudia amani kote nchini.
Wakiongozwa na Mwenyekiti wa Baraza la mashauri ya kiislam nchini KEMNAC Sheikh Juma Ngao, viongozi hao wamesema hatua ya wawili hao kuungana inalenga kuhakikisha taifa hili linapiga hatua kimaendeleo.
Akizungumza na Wanahabari katika eneo la Kombani kaunti ya Kwale, Sheikh Ngao amemtetea rais Kenyatta na kusema kiongozi huyo wa taifa ana malengo bora kwa wakenya wote.
Wakati uo huo amewahimiza wananchi kujitokeza kwa wingi na kushiriki uchaguzi mkuu wa Agosti 9 sawa na kuwachangia viongozi wenye rekodi nzuri ya maendeleo.