Story by Hussein Mdune-
Baadhi ya viongozi wa kidini mjini Mombasa wamewataka viongozi wa kisiasa kukoma kuingilia kati utendakazi wa Tume huru ya uchaguzi na mipaka nchini IEBC.
Wakiongozwa na Askofu wa Kanisa la ushindi baptist eneo la Likoni Joseph wanasiasa hawafai kuingilia utendakazi wa tume hiyo
Askofu Maisha ameshikilia kwamba ili taifa hili liweze kuwachagua viongozi waadilifu na wawajibikaji, wakenya wanafaa kuunga mkono juhudi zinazoendelezwa na tume hiyo kwani ndio njia pekee ya kufanikisha uchaguzi huru na haki.
Askofu Maisha amewataka viongozi wa kisiasa kuendeleza siasa za amani ili kuepukana na vurugu za kisiasa ifikapo uchaguzi mkuu wa Agosti 9.
Hata hivyo amewataka wakenya kudumisha amani sawa na kujitenga na viongozi wenye kuwatumia vibaya wakati huu wa uchaguzi mkuu.