Viongozi wa kidini wameombwa kutoa mwelekeo kuhusu swala la ndoa ili kuzuia dhuluma za kijinsia na mizozo ya kinyumbani miongoni mwa wanandoa Pwani.
Afisa wa maswala ya jinsia na haki za watoto katika Shirika la utetezi wa haki za kibinadamu nchini MUHURI Bi. Topista Juma amesema baadhi ya wanandoa wameshindwa kuvumiliana, hali inayochangia visa vya dhuluma na hata mauaji.
Akizungumza jijini Mombasa, Bi. Topista amesema kwamba shirika hilo limekuwa likirekodi visa kadhaa vya wanandoa kukabiliana, kudungana visu kuuwawa au hata kuwauwa watoto wasiokuwa na hatia.
Kauli ya Topista inajiri siku chache baada ya mwananume mmoja kwa jina John Maina Wang’ombe mwenye umri wa miaka 30 kuwauwa watoto wake wawili kwa kuwagonga na chuma kabla ya kuwadunga kisu vifuani na shingoni.
Taarifa Na Gabriel Mwaganjoni