Story by Bakari Ali –
Viongozi wa dini ya kikristo katika Muungano wa Mabaharia humu nchini wamezuru katika bandari ya Mombasa ili kufahamu kwa kina sababu zilizochangia kukwama kwa Meli moja kutoka taifa la Vietinam yapata takriban miezi 6 sasa.
Wakiongozwa na Askofu mkuu wa Kanisa la Katoliki jimbo la Mombasa Martin Kivuva, viongozi hao wamesema kuna takriban mabaharia 7 kutoka bara Asia waliyokwama katika meli hiyo na wanapitia mateso baada mmiliki wa meli hiyo kudinda kuangazia maslahi yao.
Askofu Kivuva amesema kumeshuhudiwa ongezeko la visa vya kuteswa kwa mahabaria ulimwenguni na wakati umefika sasa kwa wamiliki wa meli kuangazia masuala ya mabaharia.
Wakati uo huo ameitaka serikali na wadau mbalimbali katika sekta hiyo kuingilia kati suala hilo na kuwasaidia mabaharia hao kurejea nchini mwao.