Story by our Correspondents –
Padre wa Kanisa Katoliki la Holy Family Basilica jijini Nairobi David Kinyanjui awamehimiza wakenya kuungana na kuweka kanda tofauti zao za kisiasa na migawanyiko isiokuwa na msingi wowote.
Akiwahutubia waumini wa kanisa hilo wakati wa ibada ya Misa ya Jumapili, Padre Kinyanjui amesema njia pekee ya taifa hili kuafikia malengo yake kwa amani ni kuendeleza mshikamono wa jamii na uwiano.
Padre Kinyanjui amesema Kenya bado inakabiliwa na janga la Corona lakini cha kushangaza ni siasa za migawanyiko zinazoendelezwa humu nchini huku akiwataka wananchi kuungana ili kuendeleza umoja wa taifa.
Wakati uo huo amewahimiza waumini wa dini mbalimbali nchini kuhakikisha wanazingatia kanuni zote za Wizara ya Afya nchini katika kupambana na maambukizi ya virusi vya Corona ili kudhibiti msambao wa virusi hivyo.