Story by Hussein Mdune
Viongozi wa kidini katika kaunti ya Kwale wamejitokeza na kuhimiza kuheshimiwa kwa wanasiasa wanawake wakidai kwamba wana haki sawa ya kikatiba kuwania nyadhfa mbalimbali za kisiasa nchini bila ya kukandamizwa na mtu yeyote.
Viongozi hao wakiongozwa na Mchungaji wa kanisa la kianglikana eneo la Shimbahills na Lukore kaunti ya Kwale Emaryline Kyalo wamesema taifa hili linazingatia demokrasia hivyo basi wanasiasa wanawake wanafaa kupewa nafasi yao.
Mchungaji Emaryline amesema kila inapofika kipindi cha uchaguzi mkuu wanawake wanaowania viti mbalimbali vya kisiasa wameonekana kudharauliwa na kubaguliwa na wanaume wanaowania nyadhfa hizo.
Wakati uo huo amesema kuna haja ya wakaazi kupewa elimu ya umma kuhusu umuhimu wa kupiga kura wakati huu wa uchaguzi mkuu.