Story by Janet Shume-
Baadhi ya viongozi wa kidini kaunti ya Kwale wameitaka jamii kushirikiana na wadau mbalimbali ikiwemo idara ya usalama ili kukomesha visa vya utovu wa usalama katika jamii.
Wakiongozwa na Sheikh Amani Hamis Mwachirumu, viongozi hao wamesema suala la Mihadarati kupatikana kiholea limechongia kukithiri kwa visa vya utovu wa usalama hususan maeneo yanayopakana na bahari hindi ikiwemo eneo la Diani.
Kiongozi huyo wa kidini amesema kuna baadhi ya vijana wa kike wamekuwa wakitumika kutekeleza utovu huo wa usalama.
Aidha ameeleza kwamba kuna visa vinavyochipuka vya vijana wa kike kutumika na magenge ya kihalifu katika kubeba silaha katika maeneo ya watu wengi ili kuwasaidia kutekeleza visa vya kinyama.
Ameitaka jamii kutokubali kuwaficha wahalifu na badala yake kuripoti visa vyovyote vya kihalifu katika idara ya usalama ili vikabiliwe kikamilifu.