Story by Hussein Mdune –
Viongozi wa kidini hapa Pwani wameishinikiza serikali kuhakikisha inaimarisha usalama wa kaunti ya Lamu ili kuboresha shuhuli za kibiashara na uchumi.
Viongozi hao wa kidini wakiongozwa na Askofu wa Kanisa la Ushindi Baptist Joseph Maisha, wamesema kutokana na kushuhudiwa kwa mashambulizi ya kigaidi katika kaunti hiyo ni wazi kwamba usalama umelegea.
Askofu Maisha amesema kwa Sasa miradi mingi ya serikali inatekelezwa katika kaunti ya Lamu hivyo basi kuna haja ya usalama kuimarishwa zaidi.
Kauli za viongozi hao zimejiri baada ya baadhi ya wanajeshi wa KDF kuripotiwa kuaga dunia baada ya gari lao kukanyaga kilipuzi kilichozikwa ardhi katika eneo la Baure huko Lamu.