Picha kwa hisani –
Viongozi wa kidini katika kaunti ya Kilifi sasa wanataka watoto kuhusishwa kikamilifu katika maswala ya dini ili kupunguza visa vya mimba za utotoni na utovu wa nidhamu katika kaunti hiyo.
Hatua hii imejiri baada ya visa vya mimba za utotoni kuonekana kuongezeka wakati huu ambapo watoto wako nyumbani kwa muda mrefu kutokana na mpurupuko wa janga la virusi vya corona.
Wakiongozwa na Kasisi Peter Mwarabu wa kanisa la Jesus Celebration Centre (JCC) amesema kama viongozi wa kidini ni wajibu wao kuhakikisha watoto wanakua kimaadili.
Akizungumza katika eneo la tezo, Mwarabu amesema watoto wamekaa nyumbani bila shughuli yoyote tangu kuripotiwa kwa janga la corona nchini hali iliyowapelekea watoto wengi kujiingiza kwa mienendo isiyofaa kupitia kwa marafiki na mitandao ya kijamii.