Picha kwa hisani –
Padre wa Kanisa Katoliki la Holy Family Basilica kule jijini Nairobi David Mbugua, amewahimizwa wakenya kutafakari jinsi taifa hili litakavyoweza kukabiliana na swala la ufisadi humu nchini.
Akizungumza wakati wa ibada ya Misa ya Jumapili katika Kanisa hilo, Padre Mbugua amesema ili taifa likabiliana kikamilifu na swala la ufisadi basi wazazi wanafaa kuwafunza watoto wao mapema kuhusu uadilifu na kukabili ufisadi.
Padre Mbugua amesema iwapo wazazi watawajibikia swala la uadilifu kwa watoto wao basi kasumba ya ukabila katika taifa hili litapigwa vita sawia na ufisadi.
Wakati uo huo amewashauri wakenya kuheshimu maoni ya kila mmoja ili kuzuia sitofahamu za kiuongozi humu nchini.