Picha kwa hisani –
Viongozi wa kidini katika Kanisa la Kikatoliki nchini wamevunja kimya chao kuhusu ripoti ya BB1 na kutaka kufanyiwa marekebisho kwa baadhi ya vipengee.
Akizungmza wakati wa ibada maalum ya jumapili katika Kanisa la Holy Family Basilica jijini Nairobi Padri Simon Peter Kamomoe ameomba mapendekezo ya Kanisa hilo kuhusu ripoti hiyo ya BBI kuweza kusikizwa.
Wakati uo huo Padri Kamomoe ametaka fedha ambazo zingetumika kufadhili ripoti hiyo zitumike katika kusaidia kudhibiti janga la virusi vya Corona.
Aidha kiongozi huo wa Kanisa Katoliki amezidi kuwashauri wananchi kuzidi kufuata kanuni za afya ili kudhibiti kusambaa kwa maambukizi ya virusi vya Corona.