Story by Rasi Mangale –
Viongozi mbalimbali wa dini ya kiislamu wamewahimizwa Waumini wa dini hiyo kujitenga na vitendo viovu.
Kadhi wa Mahakama ya Kwale Sheikh Salim Mwaito amesema kukamilika kwa mwezi mtukufu wa Ramadhan haifai kuwa chanzo cha waumini kujiingiza katika vitendo visivyo na maadaili.
Akizungumza na Wanahabari katika majengo ya Mahakama hiyo mjini Kwale, Sheikh Mwaito amewarai waumini kutoa Zakatul fitr jinsi imani ya dini ya kiislamu inavyoeleza.
Wakati huo uo amesema wa Waumini wa dini ya Kiislamu watakaojitokeza kwa swala ya Eid wanafaa kuzingatia masharti yaliowekwa na Wizara ya Afya nchini ili kujikinga dhidi ya virusi vya Corona.