Story by Gabriel Mwaganjoni –
Viongozi wa dini ya Kiislamu katika kaunti ya Mombasa wamedhihirisha wasiwasi wao kufuatia mchipuko wa makundi ya kihalifu katika kaunti hiyo.
Wakiongozwa na Mhubiri wa Kiislamu Sheikh Abou Qattada, viongozi hao wamesema hali ya usalama katika kaunti ya Mombasa imetikiswa pakubwa na ni sharti juhudi zaidi ziidhinishwe ili kukomesha hali hiyo.
Akizungumza katika kaunti ya Mombasa Sheikh Qattada amesema wakaazi wa maeneo ya Kisauni na Likoni wanaishi kwa hofu kufuatia mchipuko ya magenge ya kihalifu, akiitaka idara ya usalama kuiwajibikia barabara hali hiyo.
Wakati uo huo amedhihirisha wasiwasi wake baada ya kubainika kwamba magenge hayo ni ya vijana wadogo wanaostahili kwenda shuleni.