Picha kwa hisani –
Viongozi wa chama cha ANC kimejitokeza na kumtaka naibu wa rais William Ruto kujiuzulu wadhfa wake.
Wakiongozwa na mbunge wa Lugari Ayub Savula viongozi hao wamesema Ruto amehujumu utendakazi wa serikali kuu kwa kupinga miradi ya maendeleo inayoidhinishwa na kiongozi wa nchini Uhuru Kenyatta.
Savula amesema kauli zinazotolewa na Ruto kwenye majukwa ya kisiasa hasa za kumkosoa Rais Kenyatta haziendani na maadili ya wadhfa wake na kwamba kauli zake ni tishio kwa mshikamano wa taifa.
Viongozi hao wa ANC wamesema haya siku chache baada ya Naibu wa rais William Ruto kujibu kauli ya rais Uhuru Kenyatta kuhusu uongozi wa taifa