Picha kwa hisani –
Viongozi katika Kaunti ya Mombasa wamepewa wito kubuni miradi mbalimbali itakayowakimu vijana pindi mradi wa ‘Kazi mtaani’ utakapokamilika.
Kamishna wa Kaunti ya Mombasa Gilbert Kitiyo amesema japo mradi huo umewasaidia zaidi ya Vijana elfu 16 katika Kaunti hiyo, unatarajiwa kukamilika mwishoni wa mwezi Disemba mwaka huu .
Kitiyo amewahimiza Viongozi wa kaunti hiyo kuja na njia mbadala zitakazo wawezesha vijana kujikimu kimaisha wakati mradi huo unatakapo fika kikomo.
Aidha afisa huyo wa utawala amesema ni jukumu la Viongozi kuwekeza katika miradi mbalimbali ili kuhakikisha Vijana wanapata mbinu za kuwakimu maishani.