Picha kwa hisani –
Viongozi mbalimbali nchini wametuma risala zao za rambirambi kwa familia ya mwendazake Simon Nyachae, aliyefariki dunia mapema leo akiwa na umri wa miaka 88.
Rais Uhuru Kenyatta, amemtaja marehemu Nyachae kama kiongozi aliyejitolea kuliwajibikia taifa hili wakati akiwa katika nyadhfa mbalimbali za kiserikali.
Naye Naibu Rais Dkt William Ruto, amemtaja Marehemu Nyachae kama aliyekuwa kiongozi tajika na aliyependa kutekeleza majukumu yake ya uongozi
Kwa upande wake Waziri wa Usalama wa ndani Dkt Fred Matiangi amesema Kenya imempoteza mkongwe wa kisiasa nchini huku akisema serikali itatangaza taratibu za mazishi baada ya kikao na familia ya Marehemu Nyachae.
Hata hivyo Mwenyekiti wa kitaifa wa chama cha Wiper Balozi Chirau Ali Mwakwere amemtaja Marehemu Nyachae kama aliyekuwa kiongozi mzalendo na aliyependa kutekeleza majukumu yake ya kiuongozi vyema.