Story by Hussien Mdune-
Mgombea wa kiti cha uwakilishi wadi ya Kinango kaunti ya Kwale kwa tiketi ya chama cha UDM Issac Beja Bora ameahidi kushirikiana na wadau mbalimbali wa sekta ya maji na kulitatua tatizo la uhaba wa maji linaloendelea kushuhudiwa katika wadi hiyo.
Beja amesema mikakati hiyo ndio itakakabiliwa na matatizo mbalimbali yanayowakumba wakaazi mashinani, akisema iwapo wakaazi wa wadi hiyo watamchagua kama kiongozi wao basi masuala mengi muhimu yatatekelezwa mashinani.
Akizungumza katika mikutano yake ya kisiasa, Beja amesema kuwa tatizo la maji katika eneo hilo limedumu kwa mda mrefu licha ya kuwepo na viongozi, akihoji kwamba kupitia uongozi wake wakaazi watashirikishwa katika meza ya mazungumzo na kuzikabili changamoto mbalimbali ikiwemo kuzikarabati barabara zilizo katka hali duni.
Wakati uo huo amewataka wakaazi wa wadi hiyo kuwachagua viongozi kwa kuzingatia sera na wala sio kuhadaiwa kupitia misingi ya vyama huku akiwataka kudumisha amani.