Taarifa na Charo Banda
Malindi, Kenya, Agosti 3 – Viongozi katika maeneo ya Malindi na Magarini wamesutwa kutokana na hatua yao ya kususia vikao vinavyoandaliwa na vijana wa maeneo hayo.
Akizungumza na wanahabari kiongozi wa vijana eneo la Magarini Zaina Gathoni amesema hatua hio imewafanya vijana kuhisi kutengwa na viongozi wao.
Bi Gathoni amesema viongozi wa kisiasa wanamtindo wa kuwatumia vijana wakati wa kampeni zao ,akisema vijana hawatakubali kutumiwa vibaya.