Picha kwa hisani –
Maseneta kutoka ukanda wa Pwani wamepinga vikali uteuzi wa wasimamizi wa taasisi mbali mbali zinazofungamana na ubaharia nchini.
Wakiongozwa na Seneta wa Kilifi Stewart Madzayo, Maseneta hao wamesema serikali inafanya uteuzi kwa kuzingatia ukabila badala ya kuwatambua wakenya wote.
Seneta Madzayo amesema licha ya idara hiyo kufungamana na maswala ya bahari hakuna hata Mpwani mmoja aliyeteuliwa kumiliki nafasi hizo.
Kwa sasa Madzayo anataka uteuzi huo kubatilishwa mara moja akisema Maseneta wa Pwani watatumia mbinu za kisheria kuupinga uteuzi huo.