Picha kwa hisani
Viongozi wa kaunti ya Kilifi wamelaani vikali tukio la siku ya Ijumaa ambapo wanamume mmoja alifariki dunia baada ya kuzama maji katika kidimbwi kimoja eneo la Kibarani kule Kilifi alipokuwa akitoroka kipigo cha polisi wakati wa masaa ya kafyu.
Viongozi hao wakiongozwa na Mbunge wa Kilifi Kazkazini Owen Baya wamekemea vikali tukio hilo na kuitaka serikali kuwachukulia hatua za kisheria maafisa wa polisi waliohusika na tukio hilo.
Kwa upande wake Mwakilishi wadi wa Kibarani John Mwamutsi amesisitiza haja ya Inspekta jenerali wa polisi nchini Hilary Mutyambai kuingilia kati swala hilo ili familia ya mwendazake ipate haki.
Viongozi hao hata hivyo wamesema iwapo hatua za kisheria hazitachukuliwa basi watalazimika kushiriki maandamano hadi maafisa waliohusika watakapochukuliwa hatua.