Picha kwa hisani –
Viongozi wa eneo la pwani wamesema ni sharti rasilimali za eneo hilo, zinufaishe kaunti za pwani kama inavyoshuhudiwa katika kaunti zengine nchini.
Mbunge wa Jomvu Badi Twalib, amesema ni jambo la kusikitisha kuona eneo la pwani na miji yake ikiwemo Mombasa ikiendelea kudorora, ilhali kuna utajiri mwingi unaotokana na bandari ya mombasa.
Twalib ametaja kaunti mbali mbali ambazo zinarasilimali kama vile mbuga za wanyama na zinanufaika na rasilimali zao, huku miji ya pwani ikiwemo Mombasa ikiendelea kusalia nyuma kimaendeleo.
Ameongeza kusema maeneo mengine ulimwenguni yenye rasilimali ya bandari yananufaika na rasilimali hizo, na ni sharti Mombasa pia inufaike na rasilimali zake.