Shirika la kijamii la KECOSCE limebaini kuwa vikao vya hamasa kuhusu athari za mauaji ya wazee miongoni mwa vijana katika kaunti ya Kilifi vimefanikiwa kwa asilimia kubwa.
Kulingana na Mkurugenzi mkuu wa Shirika hilo Phyllis Muema, kaunti ya Kilifi ilikuwa ikishughudia visa vingi vya mauaji ya wazee lakini kupitia kwa vikao hivyo vya hamasa, visa hivyo vimepungua.
Mwanaharakati huyo amewataka vijana kutafuta mbinu mwafaka za kusuluhisha mizozo na wala sio kuwauwa wazee kiholela.
Hata hivyo amedai kuwa Shirika hilo kwa ushirikiano na serikali ya kaunti ya Kilifi linalenga kuidhinisha sera maalum ya amani katika kaunti hiyo itakayotoa mwongozo mwafaka wa kusulughisha mizozo katika jamii ya kaunti ya Kilifi.
Taarifa na Cyrus Ngonyo.