Picha kwa Hisani –
Shirika la msalaba mwekundu linatarajiwa kuwapa mafunzo ya kukabiliana na majanga vijana zaidi ya miatano katika maeneo bunge yote ya kaunti ya Mombasa kabla mwishoni mwa mwaka huu.
Akizungumza wakati wa maadhimisho ya siku ya kupunguza majanga ulimwenguni,mwenyekiti wa shirika hilo kaunti ya Mombasa Mahmood Noor amesema mafunzo hayo yatasaidia umma kuthibiti athari za majanga.
Noor amesema ni jukumu la wakaazi hasa wale wanaoishi maeneo yaliokatika hatari ya kukumbwa na majanga ikiwemo mafuriko,kuchukua hatua za mapema kuepuka athari za majanga hayo.