Maafisa wa polisi eneo la Kisauni Kaunti ya Mombasa wanawazuilia vijana watatu wanaoshukiwa kuwa viongozi wa genge la majambazi la ‘Wakali kwanza’ linalowahangaisha wakaazi katika eneo hilo.
Hii ni baada ya watu wanane kujeruhiwa vibaya sana kwa kukatwa katwa kwa mapanga na kundi hilo usiku wa kuamkia leo. Majeruhi wanapokea tiba ya dharura katika hospitali kuu ya rufaa ya Ukanda wa Pwani.
Kamanda mkuu wa polisi Kaunti ya Mombasa Johnstone Ipara amesema watatu hao wanahojiwa ili kuwaelekeza polisi kule wenzao wanakojificha ili wanaswe na kukabiliwa kisheria.
Ipara amesema maafisa wa polisi wameimarisha msako mkali dhidi ya kundi hilo na itawalazimu kutumia nguvu kupita kiasi ili kulidhibiti genge hilo akiwataka wakaazi kuwafichua wahalifu wanaoishi nao katika maeneo ya makaazi.
Kwa upande wake, Afisa mkuu wa polisi wa eneo la Kisauni Julius Kiragu amewataja watatu hao kama Jackson Okelo wa umri wa miaka 26, Paul Ayub Mwabaka , miaka 18 na Ibrahim Mohammed Hamdan wa umri wa miaka 17 kama viongozi wakuu wa genge hilo na tayari wamo kizuizini.
Watatu hao wamepatikana na simu mbili na vifaa vya kuhifadhi moto yaani ‘Power banks’ na bidhaa nyinginezo zinazoaminika kuibiwa Wakaazi waliyovamiwa usiku wa kuamkia leo.
Ameongeza kuwa watatu hao wanaozuiliwa katika kituo cha polisi cha Kadzandani wamekuwa wakiwahangaisha Wakaazi kwa kuwavamia, kuwaibia na kuwajeruhi hasa katika mitaa ya Kwa bulo, Lake view, Bamburi mwisho katika Gatuzo hilo dogo la Kisauni.
Polisi wanawaandama wengine 7 wanachama wa genge hilo waliyo mafichoni
Imagine all should be brought to 📖