Maafisa wa polisi kaunti ya Mombasa wamewatia nguvuni vijana watatu wanaoaminika kuwa miongoni mwa wanachama wa makundi ya kihalifu yanayohangaisha wakaazi katika maeneo ya Kisauni na Nyali.
Kulingana na naibu kamishna eneo la Kisauni Julius Kiragu watatu hao wamenaswa katika nyumba moja eneo la Utange pamoja na mapanga matatu, simu saba za rununu na sare za polisi.
Kiragu amekiri kwamba polisi wanashindwa kuyasambaratisha magenge ya kihalifu katika maeneo ya Kisauni na Nyali kwani wakaazi wa maeneo hayo hawashirikiani na maafisa wa usalama.