Picha kwa hisani –
Vijana watatu wenye umri wa miaka 15, 16 na 17 wameaga dunia baada ya kuhusika katika ajali ya barabarani katika eneo la Ng’ombeni kaunti ya Kwale kwenye barabara kuu ya Likoni – Lunga lunga.
Kamanda wa polisi Kwale Joseph Nthenge amethibitisha ajali hio akisema vijana hao walikua kwenye pikipiki wakielekea upande wa Likoni na wamegongana ana kwa ana na lori ilikua ikielekea eneo la ukunda na kufariki papo hapo.
Nthege amesema polisi wameidhinisha uchunguzi kubaini chanzo cha kifo cha watatu hao akiwemo Ramadhan Mwakunyendeka,Sadiq Mwambawa na Salim Mwachaka.
Miili ya watatu hao kwa sasa imehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhi maiti katika hospitlai ya mjini Kwale.