Kiongozi wa vijana katika eneo bunge la Mvita Mohammed Hussein amesema licha ya idadi kubwa ya vijana kuwa na uwezo wa kubadili maisha yao katika maswala ya elimu na uongozi wamesalia nyuma wakisubiri msaada hasa utoka kwa viongozi wa kisiasa.
Hussein amesema ni sharti vijana wabadili taaswira yao maishani na wajitahidi katika nyanja mbalimbali zikiwemo za uongozi, biashara, elimu, na siasa badala ya kusalia wakilalamikia kubaguliwa.
Hussein amewataka vijana kushiriki makongamano mbalimbali yanayoandaliwa kwa ajili yao ili kujipatia habari na muongozo muhimu wa kuafikia ndoto zao maishani badala ya kupuuza vikao hivyo.