Picha kwa hisani –
Vijana katika eneo la Dabaso Kaunti ya kilifi wameonywa dhidi ya kujiingiza kwenye vurugu za uchaguzi mdogo utakaoandaliwa eneo hilo, na badala yake wawe katika mstari wa mbele kuhubiri amani.
Akitoa wito huo kwa vijana kule Gede, mshirikishi wa shirika la Haki yetu Warda Zige, amewataka vijana kukoma kutumiwa vibaya na wanasiasa wakati wa kampeni na hata kwenye uchaguzi huo mdogo.
Mshirikishi huyo aidha amehoji kuwa kwa Sasa kumeshuhudiwa joto la kisiasa hasa maeneo ya Dabaso na Mswambeni, ambako uchaguzi huo mdogo utafanyika.
vijana hao hata hivyo wameapa kuwa katika mstari wa mbele kuhubiri amani, sawia na kujitenga na vurugu wakati na baada ya uchaguzi huo.
Uchaguzi huo mdogo unatarajiwa kufanyika tarehe 15 desemba katika eneo bunge la Msambweni na Wadi ya Dabaso Kaunti ya kilifi.