Picha kwa hisani –
Mwanaharati wa vijana katika kaunti ya Mombasa Omar Chai, amewaonywa vijana dhidi ya kujihusisha katika uhalifu na utumizi wa Mihadarati kwa kisingizio cha ukosefu wa ajira.
Akizungumza kule Kadzandani katika eneo bunge la Nyali, Chai amesema ni sharti vijana watafute mbinu mbadala ya kujikimu kimaisha na wala sio kujihusisha katika uhalifu.
Kulingana na Chai, Vijana wataendelea kulalamikia ukosefu wa ajira iwapo hawatashirikiana na kujadili njia mwafaka za kujinasua kutokana na hali ngumu kiuchumi.