Picha kwa hisani
Maafisa wa polisi katika eneo la msambweni kaunti ya Kwale wanawasaka vijana wanaoshukiwa kuhusika na mauaji ya mwanamume mmoja yaliotekelezwa katika eneo la kibundani kaunti ya Kwale.
Taarifa kutoka kwa maafisa wa polisi imeeleza kwamba kundi la vijana lilimvamia mwanamume huyo aliekua mlevi kwa jina George Hezron Kotini mwendo wa saa tatu usiku hapo jana na kumpiga kwa kisingizio kwamba ana maambukizi ya virusi hatari vya Corona.
Inaafiwa kwamba polisi walifika katika eneo la mkasa na kumpata mwanamume huyo akiwa na majeraha mabaya kabla ya kumkimbiza katika hospitali ya rufaa ya msambweni amabako aliaga dunia.