Vijana wanaoshiriki uhalifu na kuwahangaisha wakaazi katika Kaunti ya Mombasa kamwe hawatasazwa katika oparesheni ya kiusalama inayoendelezwa.
Naibu Kamishna wa Kaunti hiyo Mahmoud Salim amesema vijana hao wamekuwa wakitumika na kusajiliwa katika makundi ya kihalifu akisema maafisa wa usalama kamwe hawatawasaza vijana hao bali watawakabili kikamilifu.
Wakati uo huo, Mahmoud ameisihi jamii ya Mombasa kuwafichua walanguzi wa dawa za kulevya ambao wamewaathiri pakubwa vijana.
Wakati uo huo, afisa huyo tawala amewataka wazazi kuwasajili vijana wao katika shule za kiufundi ili wapate ujuzi wa kujikimu maishani.