Picha kwa Hisani –
Kumezuka vurugu katika makao makuu ya eneo bunge la Changamwe Kaunti ya Mombasa baada ya kundi la vijana waliyotekeleza ‘Kazi mtaani’ kulalamikia kutolipwa.
Naibu kamishna eneo hilo Dennis Barasa amesema vijana hao walitoa nambari za simu zilizokuwa na dosari wakati wakisajiliwa kwenye mradi huo hali inayochangia utata huo.
Hata hivyo vijana hao wakiongozwa na Bi Sophia Mwangangi wameshikilia kwamba hawataondoka eneo hilo hadi walipwe kwa kazi waliyoifanya tangu mwezi Julai mwaka huu.
Mmoja wa vijana hao Esther Muasya amesema licha ya kurekebisha nambari zao za simu wamesubiri malipo hayo kwa kipindi cha majuma mawili sasa bila ya mafanikio yoyote.