Story by Hussein Mdune–
Mgombea wa kiti cha uwakilishi wadi ya Puma katika kaunti ya Kwale Mrinzi Nyundo Mrinzi amewahimiza vijana kuwaunga mkono vijana wenzao waliojitosa katika ulingo wa siasa.
Akiwahutubia wakaazi wa Wadi hiyo wakati wa mikutano ya kisiasa ya chama cha Wiper katika eneo Mazola, Mrinzi amesema ni lazima vijana watambue juhudi za vijana wenzao ndiposa watabadili uongozi duni.
Mrinzi ambaye anawania kiti hicho cha Wadi ya Puma kwa tiketi ya chama cha Wiper amesisitiza umuhimu wa vijana kuungana ili kupigania nafasi za ajira.
Wakati uo huo amewataka vijana kudumisha amani sawa na kujitenga na wanasiasa wenye malengo ya kuwatumia vibaya wakati huu wa kampeni za uchaguzi mkuu.