Picha kwa hisani –
Mamlaka ya barabara za mjini nchini KURA imethibitisha kuwa ukarabati wa kilo mita kumi za barabara za mji wa Hola kaunti ya Tana-river umekamilika.
Mkurugenzi mkuu wa mamlaka hio mhandisi Silas Kinoti amesema ukarabati huo ulioendelezwa kwa mwaka mmoja umegharimu shilingi milioni 542 akisema kukamilika kwa mradi huo kutawavutia wawekeza na kuimarisha mji huo.
Mhandisi Kinoti amesema mradi sawia na huo utaidhinishwa katika miji ya Mokowe-Lamu, Lodwar, Mandera na maeneo mengine nchini ili kuimarisha miji hio na kuvutia wawekezaji.
Mkurugenzi huyo wa mamlaka ya KURA amewahimiza vijana wa humu nchini Kutumia fursa ya mradi huo kupata ajira na kushiriki katika ujenzi wa taifa.