Story by Ali Chete-
Shirika la utetezi wa Haki za kibinadamu nchini HAKI Africa likishirikiana na ubalozi wa uholanzi limezindua mradi wa kuwahamasisha viongozi wa kidini ili kuhakikisha taifa linashuhudiwa amani wakati wa uchaguzi mkuu.
Msimamizi wa miradi huo kutoka shirika hilo Mesaid Omar amesema mradi huo unanuia kuwapa viongozi wa kidini nguvu za kueneza hamasa za amani kwa ikizingatiwa kwamba wanauwezo wa kufikia watu wengi hasa siku za ibada.
Kwa upande wao viongozi wa kidini wakiongozwa na Sheikh Alfan Ali wamesema mradi huo utawawezesha viongozi hao kuhimiza amani wakati huu ambapo siasa zimepamba moto huku akidokeza kwamba viongozi wa dini mbalimbali wanajukumu la kuwarai wananchi kudumisha amani.
Kauli yake imeungwa mkono na mtumishi Melzedeck Anyumba aliyewahimiza vijana kutokubali kushawishiwa vibaya na kuzua vurugu za kisiasa bali kujitokeza kwa wingi na kuwa mabalozi wa amani.