Afisa wa nyanjani wa Shirika la ‘Reachout Centre Trust, Hassan Suleiman amesema ni sharti vijana wajumuishwe katika maswala ya uongozi ili wahakikishe wanapigania haki zao.
Suleiman anasema vijana wengi wamejipata katika uraibu wa dawa za kulevya kutokana na kukata tamaa maishani pindi wanapowaona wakongwe wakishikilia nafasi za uongozi na hata kupewa majukumu mbalimbali na Serikali.
Akizungumza katika eneo la Likoni kaunti ya Mombasa, Suleiman amesema pindi vijana watakapohusishwa katika maswala ya uongozi basi watakuwa na nafasi bora katika kuwasaidia vijana wenzao ili wajikinge na maovu katika jamii.
Wakati uo huo, amesisitiza umuhimu wa Serikali za kaunti hapa Pwani kuekeza zaidi katika vijana na kuidhinisha miradi inayowalenga moja kwa moja vijana mashinani.
Taarifa na Gabriel Mwaganjoni.